Hivi Kwanini Unaitwa Hivo..
TAMKA na ANDIKA jina LAKO vizuri Kila mtu hasa vijana wengi wana majina ya utani yaani "a.k.a..."kama vile platinum, Jamaica,Anyama,Master e,n.k Mara nyingi haya tunapewa Na marafiki kutokana tabia zetu kwao au kufanania na mtu mwenye jina hilo..Wakati mwingine tunajibatiza wenyewe. Lakini bado tunapozaliwa wazazi nao utupatia majina hasa Kutokana Na hali,wakati Na hata majira ya mwaka tulipokuwa tunazaliwa Mfano "Hayo Malando,Shida,Sipendeki n.k JINA umtambulisha mtu Mfano. “Paulo mtumwa wa Kristo” (Rum 1:1-7) Saulo muuaji aliandika vizuri jina lake akawa Paulo mtumwa wa Yesu Nukuu: “Atajifungua mtoto wa kiume, nawe utampa jina Yesu, kwa kuwa yeye ndiye atakayewaokoa watu wake katika dhambi zao” (Mathayo 1: 21). Yesu ameandika vizuri jina lake. Ni mwokozi na mkombozi. Nukuu: “…‘Yozefu, mwana wa Daudi, usiogope kumchukua Maria awe mke wako, maana amekuwa mjamzito kwa uwezo wa Roho Mtakatifu..” (Mathayo 1: 18-20). Yosefu angemwacha Bikira M...