Kumbukumbu ya Uyahudi Duniani
Kumbukumbu ya Uyahudi Duniani . Madai ya Waisraeli yanaanzia katika misingi ya kidini ambapo katika Biblia ( kitabu kitakatifu kwa Wakristo na Wayahudi ), kitabu cha kwanza cha nabii Musa kiitwacho Mwanzo sura ya 12 inaonesha jinsi Ibrahim anavyoitwa na mwenyezi Mungu ili kumtumikia . Eneo hilo la Palestina ( zamani lilijulikana kama Kaanani ) ndiyo chimbuko la dini kuu tatu zenye msingi wa Ibrahim ambazo ni dini ya Wayahudi , Ukristo na baadaye Uislam . Dini ya wayahudi yenye misingi ya Biblia Agano la Kale likianza na vitabu vitano vya Musa ( Mwanzo , Kutoka , Hesabu , Mambo ya Walawi na Kumbukumbu la torati ), Ukristo ukianza misingi kwenye Agano la Kale hadi Agano Jipya na Uislam ukishika vitabu vinne Tourat ya nabii Musa ( a.s ), Zabur ya nabii Dawood ( a.s ), Injili ya Issa bin Mariam ( a.s .) au Yesu na Quran ya Muhamad ( s.a.w ) Ibrahim mwenyeji wa ...